Appel à la solidarité pour 3 étudiants comoriens qui ne peuvent pas payer leurs études à l'Université de Zanzibar. 2 jeunes femmes et...
Appel à la solidarité pour 3 étudiants comoriens qui ne peuvent pas payer leurs études à l'Université de Zanzibar. 2 jeunes femmes et 1 garçon, originaires de l'île d'Anjouan, dont l'un est en phase de finir un master d'économie. Le Mufti de l'Ile qui connait bien les Comores et a aidé les étudiants, a fait appel à des Zanzibaris d'origine comorienne. Ci-dessous le message envoyé à des membres de la communauté d'origine comorienne de Zanzibar.
1 franc comorien = 5,2 shillings tanzaniens
L' indicatif téléphonique de la Tanzanie est 00255
Par Said Mshangama
"ASALAAM ALAYKUM!
Natuma ombi hili kwenu kuomba kuwasaidia wanafunzi 3 kutoka Ndzuwani vsiwa vya Ngadzija wakiwa wanawake wawili na mmoja wao akiwa mwanamume.
Katika mwezi wa June 2018 mie Hamza Z. Rijal na Ali Aboud Mzee tuliitwa na Mufty Mkuu wa Zanzibar kupitia Katibu wake. Tuliitikia wito na aliotutaka Mufty ni kuweza kutafuta njia ya kuwasaida wanafunzi 3 wawili wanasoma Diploma Chuo cha ICPS na mmoja anafanya Master Degree in Economics katika Zanzibar University.
[next]
Mufty kupitia msemaji wake alitutaka sisi kama wana Wakfi tuweze kuwasaidia, tumekuja kuelewa kuwa Balozi wa Ngadzija aliwahi kutoa msada kwa hao wanafuzi lakini mwisho akasema kuwa mzigo umekuwa mzito kwahio hawezi kuwasaidia.
Wanafunzi hawa wamekuwa hawawezi kujikimu kwa chakula wala malazi pamoja na kulipa fedha za masomo. Wakashauriwa kuomba msada kwa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar(JUMAZA) ambao kwa upande wao waliweza kuwasaidia sehemu ya mzigo waliokuwa nao. JUMAZA mzigo ulivyokua mzito wakausogeza kwa Ofisi ya Mufti ambapo waliweza kuwasaidia na kufikia nukta ya Mufti kuwasaidia kuwalipia shida za hawa wanafunzi kutoka mfukoni mwake kwa kuwa hana kifungu cha bakejeti kuwasaidia wanafunzi, kwa upande wake bada ya kuwasaidia kwa kipindi Fulani akaona kutwita sisi kuweza kupitia Wakfu wa Wangazija kuwapatia suluhisho hawa vijana.
Jana tulibahatika kukutana na Hilma Ali Maoulida ambaye anafanya MA in Economics ametuonyesha kuwa anatakiwa alipe 2,634,500 ndio za kumalizia masomo. Kwa upande wetu mie na Ali Aboud tumekubali kuwasaidia chakula chao cha mwezi kwa watu 3 ambao wanajipikia weyewe mpakaa watapomaliza masomo yao. Malipo ya Fee ndio tunakuombeni muwasaidie kwa kila mmoja alichonacho.
Naambatanisha malipo aliolipa Hilma na anayodaiwa na barua ya maelezo kwa atayekuwa tayari kuwasaidia. Vilevile naambatanisha barua ya Ouldia Soidikiouddine na ya Abdallah Oummair hao wawili kila mmoja anadaiwa 960,000.
Ninaleta ombi kwenu kwa yoyote yule ambaye atapenda kutabaruku kwa chochote kile awasiliane na :
Hamza Z. Rijal-0777436949 au Ali A. Mzee-07774406254
Mategemeo yangu kupata ushirikiano wenu.
Asalaam Alaykum
Hamza Z. Rijal"
HabarizaComores.com (Habari Za Comores)| أخبار من جزر القمر
COMMENTAIRES